RC DKT. MAHENGE ARIDHISHWA NA UJENZI WA VITUO VYA AFYA VYA MTERA NA CHIPOGORO WILAYANI MPWAPWA, AMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUTEKELEZA AHADI YA KUJENGA KITUO CHA AFYA CHA MTERA.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameelezea kuridhishwa na hatua ya ujenzi wa vituo vya Afya vya Mtera na Chipogoro vilivyopo Wilayani Mpwapwa ambavyo vimegharimu zaidi ya shilingi Milioni 600 huku vikitarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi mwishoni mwa mwezi huu wa septemba kwa kituo cha Mtera huku kituo cha Chipogoro kikitarajiwa kuanza kutoa huduma katikati ya mwezi huu.
Dr. Mahenge akiwa ziarani Mpwapwa katikati ya wiki hii, amemshukuru Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa kwa wananchi wa Mtera mwezi Aprili, 2019 akiwa safarini kutokea Iringa kuja Dodoma baada ya kuridhia ombi la wananchi hao la kubadilisha matumizi ya majengo ya iliyokuwa kambi ya wakandarasi waliojenga barabara ya Dodoma Iringa ili yatumike kama kituo cha afya na baadae kuleta shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuongeza miundombinu ya majengo ya kutolea huduma kwenye kituo hicho cha Mtera na sasa ujenzi ukiwa ukingoni kituo kikitarajiwa kuanza kutoa huduma mwishoni mwa mwezi huu.
Dkt. Mahenge amebainisha uongozi wa Rais Magufuli ni wa vitendo na matokeo yanayoonekana ambapo amethibitisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake katika sekta ya Afya kwenye Mkoa wa Dodoma, Rais Magufuli amefanikiwa kujenga vituo vipya vya afya 26 kwa gharama ya zaidi ya bilioni 13 na hospitali 6 kwa gharama ya zaidi ya bilioni 9 jambo ambalo hapo zamani tulizoea kusubiri kwa miaka mingi kukamilisha miradi kama hii huku akibainisha kuwa bajeti ya dawa kwenye Mkoa wa Dodoma kwa sasa imeongezeka hadi kufikia bilioni 12 kwa mwaka kutokea milioni 900 iliyokuwepo wakati Rais Magufuli anaingia madrakani.
Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa
Anuani ya Posta: 914 DODOMA
Simu: +255 26 232 4343/232
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz
Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.